Description
Mwandishi wa kitabu hiki anatuletea watu wa kuiga; watu wenye tabia nzuri, watu waliotakaswa na Mwenyezi Mungu (Qur’an 33:33). Hawa ni watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w) ambao walikuwa wachamungu, wakarimu, wapole na wenye tabia nzuri ya kuigwa. Hii yote ni katika juhudi za mwandishi huyu kutaka kurekebisha tabia na mwenendo katika jamii inayotuzunguka.