Description
Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, pale umri wa mscichana unapofikia miaka tisa, anahesabiwa kuwa amefikia utu uzima (amebaleghe), kwa umbile anakuwa ama ni dhaifu au mwenye nguvu – anakuwa ni mrefu au mfupi wa kimo – na anakuwa miongoni mwa wasichana wanaocheza au mtu mwenye wajibu ndani ya nyumba.
Athari ya kwanza kabisa ya kubaleghe kwake ni kwamba, Mwenyezi Mungu baada ya kuona ubora wa hali yake ya kimwili na kiroho anampamba na majukumu yote ya Amri Zake – ya wajibu yanafanywa kuwa faradhi juu yake – makatazo (haramu) yanaharamishwa, na kwa namna hii anamjaalia mwanamke hali ya hadhi ambayo mwanamume anaipata baada ya miaka sita.