Description
Kwa hivyo, maudhui yaliyomo katika kitabu hiki ni yenye kuwafaa Waislamu wote wa madhehebu zote. Kutokana na umuhimu wa maudhui haya ambayo kwa uchache kila mwislamu anatakiwa aijue misingi hii, tumeona tuyatoe masomo haya katika lugha ya Kiswahili ili wasomaji wetu wa Kiswahili wapate kufaidika na yaliyomo katika safu hii ya masomo na kuongeza ujuzi wao katika masuala ya kidini na kijamii.