Description
Moja ya sababu ambazo Waislamu wanadai kurejeshwa kwa Mahakama ya Kadhi hapa Tanzania Bara ni kuhusu utekelezaji na hukumu za ndoa na talaka ambavyo vyote vimeanishwa katika Qur’ani Tukufu.
Kwa Waislamu, jambo lolote linapotajwa katika Qur’ani Tukufu huwa ni amri (imperative) na kwa hivyo lazima litiiwe, lifuatwe na litekelezwe vilivyo. Hii ndio maana ya kuitwa “Uislamu ni dini na ni mfumo wa maisha”, kwa maana kwamba Uislamu huhudumia roho na mwili au kwa lugha nyingine, huhudumia roho na kusimamia mambo yote yanayohusu maisha ya watu. Na huu ndio umuhimu wa Mahakama ya Kadhi kwa Waislamu sio suala la kupuuzia kwao.
Mwandishi anazungumzia utekelezaji wa talaka, inavyopaswa kutolewa na wakati gani. Maelezo na majibu ya maswali haya utayapata katika kitabu hiki. Fuatana na mwandishi.